Kama wewe ni
mtumiaji wa Mabasi ya mwendokasi Dar es salaam hasa upande wa Kariakoo inabidi
ujue siku ya leo Jumatano January 25 Rais Magufuli anaweka baraka zake kwenye
mradi huo hivyo safari za kuingia na kutoka zitasimama kwa muda.
Deus
Buganywa kutoka UDART amesema ‘uzinduzi wa mradi utafanywa na Rais Magufuli na
kutokana na shughuli hiyo kufanyika Mtaa wa Gerezani, tutasitisha kwa muda
huduma za mabasi yanayotoka FIRE kuja GEREZANI kati ya saa 4 asubuhi mpaka saa
7‘
Watanzania walio wengi wanamjua Mh. Rais ni kipenzi cha
wanyonge na anatekeleza ilani kwa vitendo... na anasimamia ile dhima ya chama
Binadamu wote sawa na kila mtu lazima afurahie mafanikio ya nchi yake.
Nimekubali Mh. Rais anapendwa had wamachinga wote wameacha
biashara kwenda tu kumshangilia. Tanzania mpya naiona kwa kweli.
Pia uzinduzi huu wa mabasi haya ya mwendo kasi yatakua ni
ukombozi mkubwa sana katika barabara ya kutoka kariakoo na kuelekea maeneo
mengine ya jiji la Dar es Salaam
Tunakushukuru sana Mh. Rais... Tuna imani nawe na
tunakupenda na kukuombea Mpendwa wetu. Hapa Kazi Tu.
Toa Comments yako hapa tuijenge Tanzania yetu. Jiunge na E
Gossip 5 sasa kupata habari mpya kila siku.
Post a Comment