
Ripoti mpya kutoka The Independent na ParsToday zinasema
kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo
kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa ambapo uamuzi huo
umefanyika katika siku yake ya kwanza kazini.
Trump ambaye aliapishwa Ijumaa January 20, 2017 kuwa Rais wa
45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtangulizi wake, Barack
Obama kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muda wa kujitayarisha kuondoka
kama ilivyo kawaida.
Inaelezwa kuwa zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi
mbalimbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana
ikiwa ni mara baada ya Trump kuapishwa.
Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na
washirika muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza na Canada ambapo ripoti
zinasema nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya
Trump kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress
kabla ya kuanza kazi zao.
Donald Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na
hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za serikali ya Marekani na haya yanajiri
huku maandamano yakiripotiwa kuendelea sehemu mbalimbali kupinga utawala wa
kiongozi huyo.
Nchini Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump
kumeripotiwa maandamano ya watu milioni tatu na imeripotiwa kumefanyika
maandamano 637 katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais huyo
mpya wa Marekani.
Post a Comment