Sasa hivi ni
zaidi ya miezi mitatu toka tusikie kuwa Rappa Nay wa Mitego na
aliyekuwa Producer wake wa zamani Mr T Touch waache kufanya kazi
pamoja,mwanzoni wakati studio ya Free Nation inafunguliwa, Nay wa
Mitego alisema kuwa studio hiyo ameamua kumfungulia Producer wake kama zawadi
kwa kumtengenezea hits nyingi.
Katikati ya
mwaka jana tulisikia kuwa wamegombana na Nay wa Mitego akaamua kuichukua
studio hiyo na kuihamisha ilipokuwa mwanzo na kuipeleka sehemu nyingine,sasa
hivi studio hiyo imekamilika na Nay wa Mitego katuonyesha kwa ndani
ilivyo.
Kupitia
akaunti ya Instagram ya Nay wa Mitego ameshare picha ambazo zinaonyesha
kukamilika kwa studio hiyo na tayari inaonekana imeshaanza kufanya kazi.
Post a Comment